
Kwa mnunuzi
Tafuta bidhaa.
Uliza Kika, pata bei.
Unatafuta kitu? Uliza kwa Kiswahili — pata bei na duka lililo karibu, popote Tanzania.
Msaidizi wako wa manunuzi
Ni kama kumtuma ndugu mjini — ila kwa WhatsApp. Duka lolote Tanzania, hata lisilo na app wala website: Kika inalitafuta, inauliza bei, na ukiagiza — unachukua dukani, au duka linakuletea kama linasafirisha.
Bure kuanza · Dakika 2 · Hakuna app mpya
Inaendeshwa na Google Gemini · MedGemma

Kwa mnunuzi
Uliza Kika, pata bei.
Unatafuta kitu? Uliza kwa Kiswahili — pata bei na duka lililo karibu, popote Tanzania.

Kwa biashara
Ona faida yako.
Invoice, madeni, stock, matumizi na faida — kisha fungua Portal kuona kila kitu.
Tiketi za safari, vipuri vya gari, dawa, na simu halisi ya Kika dukani. Telezesha uone zaidi.
Boti, treni ya SGR, basi na events. Watu watano wanaomba, Kika moja inajibu.
Rekodi halisi: Kika inauliza bei, stock na malipo ya vipuri vya Toyota IST.
Juma alituma picha ya kipuri kwa Kika. Abdallah alipanda boda. Nani alimaliza kwanza?
Neema aliona krimu Instagram. Kika ilitambua jina lake na kupata duka la dawa Mikocheni.
Layla alipewa bili ya milioni 2. Kika ilipiga simu maduka: vipuri halisi kwa milioni 1.2.
Msaidizi mmoja mahiri — kwa maisha ya kila siku na kwa biashara. Bofya kuona kila kitu.
MedGemmaTuma picha ya tatizo — Kika inachambua, inashauri dawa & duka la karibu.

Uliza bidhaa yoyote — Kika inakupa maduka, bei bora na picha.

Basi, boti ya Zanzibar na Pemba, treni ya SGR, events — tiketi inaingia WhatsApp.

Tambua kwa VIN/aina ya gari — ukweli kama kipuri kinafaa.

Angalia faini za TPF na bima ya TIRA — na upate kumbusho.
Hii ni michache tu — Kika ina uwezo 30+. Uliza tu kwenye WhatsApp.
Jinsi inavyofanya kazi
Kwa Kiswahili au Kiingereza, kama unavyoongea — hata ujumbe wa sauti.
Inaelewa, inachambua picha, inatafuta, na inapiga simu maduka kwa niaba yako.
Jibu wazi, nyaraka tayari, na hatua ya kukamilisha — papo hapo.
Usalama & Uaminifu
Teknolojia ya kisasa, iliyojengwa kwa kuaminika na kwa mazingira ya Tanzania.
Mazungumzo yako yamo ndani ya WhatsApp yaliyosimbwa (end-to-end). Hatuuzi taarifa zako.
Kika si daktari wala wakili — inatoa mwongozo wa awali, na kukwambia wazi lini kuona mtaalamu.
Kwa timu za duka, kila kitu kinabeba nani alifanya nini na lini — kinga dhidi ya upotevu.
Nyaraka rasmi zenye TIN & VAT, BRELA, zabuni za NeST — kwa mujibu wa sheria za hapa.
Matokeo
Sema tu unachotaka. Kika anakutengenezea invoice na risiti nadhifu — na nembo yako — tayari kutuma kwa WhatsApp au kama PDF.

Orodha kamili ya bidhaa, idadi na bei — jumla zikijipiga zenyewe.

Yenye jina la duka, anwani na jumla kuu — tayari kumpa mteja.
Kila hati hutoka kama PDF — na nembo yako juu.
“Nilipiga picha ya mzigo mzima kutoka Dubai — Kika ikanitengenezea invoice na jumla sahihi. Kazi ya usiku mzima, dakika mbili.”
“Nauliza tu ‘nani ananidai’ na Kika inaniletea orodha kamili. Sina tena madaftari mengi.”
“Mtoto alikuwa na tatizo la ngozi. Nilituma picha, Kika ikanieleza na kunitafutia dawa duka la karibu. Nilistarehe.”
Bei
Kila namba mpya ya WhatsApp inaanza na tokeni 700,000 bure mara moja. Hakuna ada ya mwezi, hakuna kadi ya benki. Bei ni moja kwa wateja na kwa maduka.
Anza bure
Wateja na maduka, kwenye WhatsApp
Matumizi yanategemea ombi lako. Andika salio kwenye WhatsApp kuangalia.
Ongeza tokeni
Tokeni zikiisha, Kika inakutumia vifurushi hivi kwenye WhatsApp. Unachagua kimoja, unalipa kwa simu, unaendelea.
Kikapu chako
1,000,000 tokeni
Jumla: TSh 20,000
Thibitisha namba ya kulipia kwenye WhatsApp. Tokeni zinaingia baada ya malipo kuthibitishwa.
Malipo kwa pesa ya simu: Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa kwa ombi la malipo kwenye simu yako; M-Pesa kwa Lipa Namba ya Kika. Ukinunua bidhaa au tiketi kupitia Kika, unaona jumla kamili kabla ya kulipa.
Tunajenga Kika kwa ajili ya Tanzania: msaidizi mmoja kwenye WhatsApp unaofanya kazi halisi, kwa Kiswahili.

Mwanzilishi · Mkurugenzi Mtendaji
Alizaliwa Tabora, akakulia Dar es Salaam. Alijifundisha kuandika programu kwa YouTube baada ya shule, akasomea Computer Science huko Texas, na amejenga mifumo ya malipo kwa miaka. Anaongoza bidhaa na teknolojia ya Kika.
LinkedInMkurugenzi wa Fedha
Anaongoza fedha za Kika: malipo, gharama na mipango ya ukuaji.
Unataka kujenga Kika nasi? Angalia nafasi za kazi
Maswali