Faragha
Sera ya Faragha
Kika inafanya kazi ndani ya WhatsApp. Hii ndiyo taarifa tunayokusanya, kwa nini, na jinsi ya kuiondoa.
Taarifa tunazokusanya
Ili kukuhudumia, tunakusanya na kuhifadhi:
- Nambari yako ya simu na jina lako la WhatsApp
- Mazungumzo yako na Kika
- Picha unazotuma kwa ajili ya kutafuta bidhaa
- Eneo lako — ukitoa ruhusa — ili kupata maduka karibu nawe
- Kwa wafanyabiashara: taarifa za biashara (jina, BRELA, aina, eneo)
- Kwa wafanyabiashara: hati unazozalisha, nembo na muundo wa hati zako
Tunavyozitumia
- Kukutafutia bidhaa na bei kutoka maduka yanayofaa
- Kuboresha huduma yetu
- Kutengeneza na kuhifadhi hati za biashara yako
- Kukutumia taarifa muhimu kuhusu huduma
Hatuuzi taarifa zako kwa mtu yeyote. Tunawasiliana na maduka kwa niaba yako pale tu unapotafuta bidhaa.
Zinapohifadhiwa
Taarifa zako zinahifadhiwa kwa usalama kwenye seva zilizoko Ulaya (EU), kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania, 2022.
Haki zako
- Kujiondoa: andika "stop" au "acha" kwenye WhatsApp wakati wowote
- Kufuta taarifa: tuombe tuondoe taarifa zako zote kwenye mfumo wetu
- Kupata nakala: una haki ya kuomba nakala ya taarifa zako
Kwa lolote kati ya haya, tuandikie info@kikapay.co.tz.
Masharti ya Huduma
Sera hii inakwenda pamoja na masharti yetu ya huduma, ambayo unayakubali ndani ya WhatsApp. Soma Masharti ya Huduma.
KikaPay Technologies Limited · Imesajiliwa BRELA Tanzania