Tiketi ya basi Arusha kwenda Dar es Salaam

Mwambie Kika tarehe yako ya kusafiri Arusha kwenda Dar es Salaam. Kika inatafuta mabasi yanayouza viti online siku hiyo, inakuonyesha muda, daraja na bei, unachagua kiti, unalipa kwa simu, na tiketi inaingia kwenye WhatsApp yako. Huna haja ya kwenda stendi wala kupakua app.

Kata tiketi Arusha – Dar es Salaam →

WhatsApp +255 651 059 040

Jinsi ya kukata tiketi kwa dakika mbili

  1. 1Tuma "Arusha kwenda Dar es Salaam" na tarehe kwa Kika kwenye WhatsApp.
  2. 2Kika inakuonyesha mabasi ya siku hiyo: muda wa kuondoka, daraja (VIP, Luxury, ya kawaida) na bei.
  3. 3Chagua basi na kiti; Kika inakishikilia kwa ajili yako.
  4. 4Weka PIN kwenye simu yako: M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa.
  5. 5Tiketi (PDF) inaingia kwenye WhatsApp yako. Kika inakukumbusha kabla ya safari na unaweza kufuatilia basi lako.

Mabasi mengi, chat moja

Kika inalinganisha mabasi yanayouza viti online kwa njia yako, badala ya kupiga simu ofisi moja moja.

Lipa kwa simu yako

Malipo yanaanzishwa moja kwa moja kwenye simu yako; Kika haikuombi kutuma pesa kwa mtu.

Tiketi kwenye WhatsApp

Tiketi rasmi ya basi inaingia kwenye chat yako. Ukiipoteza, mwambie Kika ikutumie tena.

Fuatilia basi lako

Familia yako inaweza kuona basi liko wapi, na Kika inakukaribisha unapofika.

Maswali ya mara kwa mara

Nawezaje kukata tiketi ya basi Arusha kwenda Dar es Salaam online?
Fungua WhatsApp, mwandikie Kika (+255 651 059 040) "Arusha kwenda Dar es Salaam" na tarehe. Kika itakuonyesha mabasi, viti na bei; unachagua, unalipa kwa simu na tiketi inaingia WhatsApp.
Nauli ya basi Arusha kwenda Dar es Salaam ni shilingi ngapi?
Nauli inategemea basi, daraja (VIP, Luxury au ya kawaida) na tarehe. Kika inakuonyesha bei halisi ya kila basi la siku yako kabla ya kulipa.
Nalipaje?
Kwa simu: M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa. Unaweka PIN kwenye simu yako mwenyewe.
Tiketi inakuja vipi?
Tiketi ya basi (PDF) inaingia kwenye WhatsApp yako mara malipo yakithibitishwa. Unaionyesha kondakta au ofisini.
Kuna app ya kupakua?
Hapana. Kila kitu ni ndani ya WhatsApp uliyonayo tayari. Kuanza ni bure.
Naweza kukata tiketi ya mtu mwingine?
Ndiyo. Mpe Kika jina kamili la msafiri na namba yake; tiketi inakuja kwako na unaweza kumtumia.

Njia nyingine za basi